CHANGIA KUSAIDIA WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
Huitaji kikubwa au kingi ili utoe, kutoa ni moyo. Tunahitaji kutambua matatizo ya wengine wenye na kuchukua hatua ya kusaidia hata kwa kidogo ulichonacho. Ili kuwa na nchi yenye uchumi imara na jamii yenye ustawi, ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba kila mtu anapata huduma sawa za afya, elimu, lishe bora. Hiyo si kazi ya serikali pekee, ni wajibu wa kila mwanajamii,tunahitaji kushirikiana kwa kidogo chetu ili tuweze kuwashika mkono wenye uhitaji na kuwasaidia tulichonacho.
Unaweza kushiriki kuchangia kidogo ulichonacho ili kusaidia makundi maalumu ya watu wasiojiweza kama watoto, wazee na akina mama. Changia kidogo chako kupita namba msimbo iliyopo kwenye ukurasa wa tovuti hii, au tumia lipa namba ya mtandao wa Tigopesa.

