DIRA
Kuwa na jamii yenye uhakika wa huduma bora za afya, maarifa (elimu), mazingira rafiki na ustawi wa kiuchumi.
DHIMA
Kusaidia watu kufahamu kuhusu matatizo mbalimbali yaliyopo katika jamii na kuweza kuwaleta pamoja ili waweze kujitoa na kuchangia katika kumaliza matatizo hayo ili kufikia kesho iliyo bora kwa kila mtu.
KUHUSU TAASISI YA KIDOGO KIDOGO
Maisha ya watu wengi yako hatarini kwa sababu wameshindwa kumudu gharama za matibabu. Wengi wamepoteza uhai kwa kukosa fedha kidogo tu.
Waanzilishi wa taasisi hii wamekuwa wakisaidia watu, wengi wao wakiwa watoto kuweza kupata matibabu, elimu na masuala mengi yanayoweza kuwafanya waishi. Kiu ya kutaka kuendelea kuokoa maisha ya wengi zaidi, ilipelekea kusajiliwa kwa taasisi hii.
Baada ya kusajiliwa kwa kuzingatia sheria na taratibu, taasisi hii inaleta watu pamoja ili kuweza kuchangia na kuweza kuokoa maisha ya wengi wenye uhitaji. Maisha ya wengi yataokolewa, kipaumbele kikiwa wanawake na watoto.
Taasisi hii pia inalenga kusaidiana na Serikali na wanajamii wote katika kuboresha huduma za afya, elimu na kupambana na umaskini.